Mradi wa ujenzi wa jengo la
Maabara katika hospitali ya Wilaya ulianza tarehe 25/12/2012 kwa ufadhili wa watu wa Marekani
kupitia taasisi yake ya Centers of Disease Control & Prevention (CDC) chini
ya Mkandarasi SALEM CONSTRUCTION LTD wa
Dar es Salaam ikiwa na malengo ya kuboresha miundombinu kwa ajili ya
upatikanaji wa huduma bora za maabara katika hospitali sita za wilaya nchini.
Hospital nyingine ni Bagamoyo (Pwani), Ludewa (Njombe, Siha (Kilimanjaro),
Karume (Kilimanjaro) na Micheweni (Pemba).
Jengo la maabara lilikamilika rasmi mnamo tarehe 25/3/2013 kwa gharama
ya dola za kimarekani 550,000 sawa na shillingi za kitanzania 880,000,000.
Wilaya ya ukerewe ni kati ya
wilaya saba (7) zinazounda mkoa wa Mwanza. Wilaya ina eneo la kilometa za mraba
6400 ambazo nchi kavu ni kilometa za mraba 640 na kilometa za mraba 5760 ni
maji ya ziwa Victoria linalotuzunguka. Wilaya inaundwa na Visiwa 38 kati ya
hivyo ni Visiwa 15 tu vyenye makazi ya kudumu na 23 ni makazi ya muda kwa
wavuvi. Kiutawala wilaya imegawanyika katika Tarafa nne (4), Kata 24 na vijiji
73. Idadi ya wakazi ni 345,147.
Makusudi ya Mradi huu wa ujenzi
wa jengo la Maabara ni kupunguza msongamano wa wagonjwa katika jengo dogo la
Maabara lililokuwa linatumika hapo awali, ambako lilikuwa na chumba kimoja tu
cha kuchukulia vipimo pamoja na kuongeza wigo wa utoaji wa vipimo zaidi na kupelekea
kupata huduma bora za afya (Quality health services delivery). Maabara hii inatumika katika Hospitali ya Wilaya
ambayo ni Hospitali ya rufaa kwa vituo 35
katika wilaya yenye jumla ya wakazi wapatao 345,147 na
ukizingatia umbali na ugumu wa usafiri katika Visiwa.
Maabara hii mpya inayo nafasi ya
kutosha na jumla ya vyumba ishirini (20) vilivyofuata ramani iliyothibishwa na
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Maabara pia ina uwezo wa kudumia wagonjwa
zaidi ya 160 kwa vipimo mbalimbali kwa wakati mmoja. Aidha vipimo mbalimbali
vya VVU na UKIMWI vitafanyika kwa urahisi zaidi kwa vyumba vilivyotengwa,
ambapo wilaya ina kiasi cha asilimia 5.1 ya maambukizi na tayari zaidi ya watu
3874 wanaoishi ya virusi vya Ukimwi wapo kwenye huduma za tiba (yaani CTC) wakiwemo
watoto 173.
Tofauti na kabla ya jengo hili,
vipimo vipya vitakavyopimwa katika maabara hii mpya ni pamoja na;
Kupanda na kuotesha vimelea (Culture and Sensitivity)
Kupima vichocheo vya viungo (Enzymes)
Kuhakiki ugonjwa wa kisukari (Glucose Tolerance Test- G.T.T)
Kifua Kikuu kwa kutumia darubini maalum
Kupima Fungasi
Kutenganisha na kutambua aina ya bacteria
Homa ya matumbo (Typhoid)
Vidonda vya tumbo
Magonjwa ya viungo (Rheumatoid factor)
Upimaji wa muda wa kutoka na kuganda kwa damu (bleeding and clotting time)
Kuhakiki kaswende kwa njia maalum ( Treponema Pallidum Hemaglutination Assay – TPHA)
Kuhifadhi sampuli za vipimo mbalimbali kabla ya kupelekwa kwa Mkemia Mkuu wa serikali (Histopathology)
 |
The Lab on outside view |
 |
This project is funded from the American People in a collaboration with CSSC |
 |
Lab Manager on Reception |
 |
Main Lab |
 |
Safety Cabinet |
 |
Refrigerators |
 |
CD4 Machine |
 |
Microscope and Biochemistry Machine |
 |
Haemotology Machine |
 |
Safety Cabinet at TB Unit |
 |
Eye wash Station |
 |
Fire Extinguisher
|
 |
Ukerewe Lab Staffs on duty |
 |
Microscope |
 |
Haematology Machine
at work |
 |
Side view of the Building |
 |
Front View of the building |
 |
CSSC Staffs from left Dr. Msuka, Madina, Dr. Sekule and the last Dr. Suka |
 |
Waiting for President Kikwete |
 |
Dr. Mbwambo CSSC Zone Manager on right and Ukerewe Hospital staff |
 |
Ukerewe Hospital Staffs |
 |
President Kikwete signing on guest book |
 |
President Kikwete listening to the CSSC Zone Manager's Speech |
 |
President Kikwete on Speech |
 |
President Kikwete |
 |
Mr. President Opening up the Lab |
 |
From Left CSSC Zone Manager Dr. Mwambo, President Kikwete and Ukerewe DMO Dr. Mataka |
 |
Mr. Emmanuel- CSSC Lab Advisor narrating Mr. President on Lab safety before the tour |
 |
President on Special Dress (Lab coat) |
 |
Mr. Pius Msekwa retired Speaker |
 |
The tour is over |
 |
The President waving to Ukerewe residents |
 |
President Kikwete and Mr. Ndikilo RC |
No comments:
Post a Comment