Is the new simplified life-long antiretroviral therapy (Option B+) for all pregnant and breastfeeding women living with HIV. The new treatment is in the form of one pill, taken once a day (compared to the previous treatment of up to six pills per day).This treatment can be provided at the community level, at local primary care facilities. It keeps mothers healthier, as they continue taking it even after giving birth, through breastfeeding and beyond. CSSC ART program expect massive expansion of the treatment coverage for both pregnant and breastfeeding women living with HIV.
Wednesday, April 30, 2014
Tuesday, April 29, 2014
Inauguration of Option B+: Zero infants HIV infections
PMTCT Clinic |
CSSC Regional Coordinator Dr. Bendela, ART Program Manager Dr. Sekule CSSC Executive Director and Director of Health Services Dr. Balati welcoming Nyamagana DC: Mr. Baraka Konisaga |
Guest of Honor arriving at Sekoutoure ground |
Inauguration of the CD4 Facs Calibur Machine at Sekoutoure Hospital which supported by CSSC |
CSSC PMTCT Officer: Njiimia Mrema welcoming the Guest of Honor to the Counseling room |
CSSC Director of Health: Dr Josephine Balati |
CSSC Executive Director Mr. Peter Maduki |
CSSC Team: From left Edgar, Lesilwa, Dr. Makongwa, Matafu, Maombi, Dr. Bendela and Kamonga |
CSSC Executive Director: Mr. Maduki greet Mwanza RC Eng. Ndikilo |
Lega Martin: A woman who is HIV positive testify safe delivery of the kid without HIV infection |
Easter Joseph: Testimonies continue |
Dr. Msangi |
Nyamagana DC: Baraka Konisaka welcoming the Guest of Honor |
Mwanza RC Engineer Ndikilo during the speech |
Mwanza RC Engineer Ndikilo pressing the alarm as a sign of inaugurating Zero infants HIV infection |
Upendo Daima Choir singing special HIV song |
Dr. Mbwambo: CSSC Lake Zone Manager |
RC leaving the Sekoutore Hospital ground |
Uzinduzi wa ZIRO VVU kwa watoto Kanda ya Ziwa
Maandamano ya uzinduzi wa Ziro VVU kwa watoto Mwanza yaliyoanzia viwanja vya Nyamagana hadi Hospitali ya Mkoa ya Sekoutoure
Friday, April 25, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
UZINDUZI WA
KAMPENI MAALUM YA KUTOKOMEZA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KUTOKA KWA MAMA
MJAMZITO AU ANAYENYONYESHA KWENDA KWA MTOTO (OPTION B PLUS)
HOSPITALI YA
MKOA SEKOUTOURE- MWANZA, JUMANNE 29 APRILI, 2014
UTANGULIZI
Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii
Tanzania (Christian Social Services Commission – CSSC) ilianzishwa mwaka 1992,
kwa ushirikiano kati ya makanisa ya Kiprotestant yaliyoko chini ya Jumuiya ya
Kikristo Tanzania (CCT) na yale yaliyo chini ya kanisa Katoliki (TEC). Lengo
likiwa ni kuwa na chombo maalumu cha kuratibu na kusimamia utoaji wa Huduma
bora za afya na elimu kupitia taasisi zilizo chini ya makanisa hayo ili kuongeza
ufanisi na ubora wa utoaji Huduma kwa Jamii.
CSSC ni taasisi inayoamini na kufuata
sera ya kufanya kazi kwa ubia au mashirikiano (Public Private Partnership -
PPP) na serikali katika kuboresha utoaji wa huduma bora ya afya katika Jamii.
MCHANGO WA CSSC KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI TANZANIA
CSSC ni chombo chenye mchango mkubwa
sana katika utoaji wa Huduma za afya na elimu nchini. Wakati CSSC ikichangia
28% ya utoaji Huduma katika sekta ya elimu nchini, kwa upande wa afya, taasisi
binafsi zinachangia 36% katika utoaji wa Huduma za afya nchini. Katika ngazi ya
halmashauri za wilaya taasisi za makanisa huchangia 62% katika utoaji Huduma za
Hospitali na huchangia 56% ya utoaji Huduma hizo za hospitali katika maeneo ya
pembezoni zaidi wanakoishi maskini zaidi nchini Tanzania. Kwa upande wa vyuo
vya utabibu mchango wa taasisi za makanisa si haba kwani kati ya vyuo vya
Manesi 134 vilivyopo nchini, 68 ni vya taasisi binafsi ambapo kati ya hivyo 44
ni vya makanisa. Kati ya vyuo 8 vya madaktari nchini 6 ni vya taasisi binafsi 4
vikiwa vya makanisa. Kati ya wanafunzi 7,458 wa vyuo vya utabibu nchini
waliodahiliwa mwaka wa masomo 2011/12, wanafunzi 5,209 walikuwa katika vyuo vya
makanisa. Kwa takwimu za mwaka 2008 vyuo vya Manesi vinavyoendeshwa na makanisa
vilikuwa vinazalisha 54% ya Manesi wote nchini (MoHSW 2011; CSSC Database 2009
-20013; HSSP III MTR report 2013).
MAPAMBANO YA KUPIGA VITA VIRUSI VYA UKIMWI
Kati ya
shughuli zinazofanywa na Taasisi yetu (CSSC),ni kushiriki katika mapambano ya
kupiga vita Virusi vya UKIMWI na UKIMWI hapa mkoani Mwanza na nchini kwa
ujumla.Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii kupitia mradi wake wa ART inaratibu
huduma ya kutokomeza maambukizi toka kwa
mama kwenda kwa mtoto,huduma za tiba kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI
(WAVIU) katika wilaya zote za mkoa wa Mwanza,wilaya ya Rorya mkoani Mara na
mkoa wa Geita ambao tutaanza kuhudumia ifikapo Oktoba Mosi mwaka huu.
Kampeni ya kutokomeza maambukizi ya
virusi vya UKIMWi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ilizinduliwa na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete mwaka 2012.CSSC kwa kushirikiana na Wizara ya
afya inatekeleza mradi huu kwa kutoa huduma za upimaji wa mama
wajawazito,wanaonyonyesha na watoto waliozaliwa na mama wanaoishi na virusi vya
UKIMWI (VVU),utoaji dawa na kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kujua hali
ya maambukizi ya VVU, mkazo pia unatolewa juu ya ushirikishwaji wa wanaume
katika suala zima la kuzuia maambukizi ya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Katika kutekeleza jukumu hilo CSSC
kwa kushirikiana na wizara ya Afya inaendelea kutoa ya mafunzo kwa watoa huduma
ya afya katika vituo vya kutolea huduma vya mkoa wa Mwanza, ambapo mpaka
sasa,watoa huduma wapatao 557 wa kutoka vituo 222 wameshapewa mafunzo ya
kutokomeza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa motto Mkoani Mwanza.
Hii ni sawa na asilimia 87.4 ya Idadi ya
vituo vya afya na watoa huduma
waliotakiwa kupewa mafunzo haya kwa mujibu wa muongozo wa Wizara ya
Afya. Kufikia Desemba 2013 jumla ya vituo 149 vilishaanza kutoa huduma ya
option B plus. Ambapo jumla ya wamama 704 ( wajawazito 560 na wanaonyonyesha
144) walipatiwa huduma.
UZINDUZI WA OPTION B PLUS MKOANI MWANZA
CSSC kwa kushirikiana na RHMT chini
ya uongozi wa mganga mkuu wa mkoa inatarajia kufanya uzinduzi rasmi wa OPTION B
Plus mkoani Mwanza tarehe 29/4/2014. Malengo makuu ya uzinduzi huo ni;
- Kuhamasisha na kuongeza
uelewa kuhusu OPTION B PLUS katika jamii
- Kutambua mchango wa watoa
huduma wa afya na kuinua ari katika kutekeleza mpango huu
Wakati uzinduzi huu kutakuwa na
maandamano (yatakayo anzia katikati ya mji hadi viwanja vya Hospital ya mkoa –
Sekou Toure),utoaji wa huduma ya mama na mtoto,shuhuda kutoka kwa wamama
wajawazito wanaoishi na VVU ( expert Mothers),hotuba ya mgeni rasmi,risala
kutoka kwa wadau mbalimbali wanaotoa
huduma ya kupambana na UKIMWI pamoja na ujumbe wa option B plus kupitia vikundi
vya ngoma vya uelimishaji.
HITIMISHO:
Uzinduzi wa OPTION B+ utasaidia
wananchi kujua umuhimu wa huduma hii, hivyo wale waliopo katika huduma hiyo,
tuna uhakika wataendelea kuitumia na kwa wale ambao hawajaingia katika mpango
huu, watahamasika na kuanza kutumia huduma hii. Wito wetu kwenu ninyi waandishi
wa habari ni kuwaomba kuhamasisha jamii kuona umuhimu wa huduma hii, ile wale
tayari wanamaambukizi wajitokeze sehemu husika kupata huduma. Pia Kuhamasisha watu wajitokeze kwa wingi katika siku
ya uzinduzi rasmi wa huduma hii tarehe 29 April, 2014 katika viwanja vya
Hospitali ya mkoa Sekoutoure.
Ahsanteni sana.
Renatus Sona
Afisa
Uhusiano
Tume ya
Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC)
TUME YA KIKRISTO YA HUDUMA ZA JAMII TANZANIA CHRISTIAN SOCIAL SERVICES COMMISSION (CSSC) TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Subscribe to:
Posts (Atom)